Tafakari ya Dominika ya 23: "Walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu..."
Katika Injili ya Dominika hii Yesu anatufundisha namna ya kumrudisha ndugu aliyekosa: kwa upendo, kwa unyenyekevu na kwa pamoja kama Jumuiya.
Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo ni mahali pa kwanza pa kuishi Neno hili — tukiombeana, tukisaidiana na kusameheana.